28 Juni 2025 - 22:24
Madrasat Hazrat Zainab (SA) - Kigamboni | Imam Hussein (A.S) ni Mlango wa Rehema Pana ya Mwenyezi Mungu

Imam Hussein (A.S) alikuwa ni mfano wa rehema ya Mwenyezi Mungu duniani. Mapambano na msimamo wake ni darasa kwa Umma. Kwa hiyo: 1_Waislamu waitikie wito wa Imam Hussein (A.S). 2_Waonyeshe huruma kwa wengine. 3_Watubu na wafanye toba kwa kupitia Ahlulbayt ili kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Madrasat ya Mabinti ya Hadhrat Zainab (SA) - Kigamboni, Dar-es-salaam - Tanzania inaendelea na Darsa mbalimbali kuhusu Imam Hussein (as) na Mapinduzi ya Karbala. Mada zilizosheheni mafunzo mbalimbali zinatolewa kupitia Walimu na Wanafunzi wa Chuo hiki cha Kidini kinachowalea Wasichana wa Kiislamu katika maadili Safi ya Kiislamu. Moja ya mada muhimu ya Leo ni mada hii kwambaImam Hussein (A.S) ni Mlango wa Rehema Pana ya Mwenyezi Mungu.

Madrasat Hazrat Zainab (SA) - Kigamboni | Imam Hussein (A.S) ni Mlango wa Rehema Pana ya Mwenyezi Mungu

🔹 Sehemu ya Kwanza:

Rehema ya Mwenyezi Mungu

  • Mwenyezi Mungu ana sifa nyingi, na Sifa muhimu zaidi ni Rehema – Yeye ndiye "Ar-Rahman" na "Ar-Rahim".
  • Na ndiyo maana karibu kila sura ya Qur'an huanza na Bismillahir Rahmanir Rahim, isipokuwa sura At-Tawba.
  • Mwenyezi Mungu ameonyesha rehema yake kupitia Mitume (saww) na Maimamu (as) – ambao ni mfano wa wazi wa rehema ya Mwenyezi Mungu juu ya viumbe wake.

Madrasat Hazrat Zainab (SA) - Kigamboni | Imam Hussein (A.S) ni Mlango wa Rehema Pana ya Mwenyezi Mungu

🔹 Sehemu ya Pili 

Imam Hussein (A.S) – Ni Mlango wa Rehema ya Mwenyezi Mungu

  • Katika maneno ya ziara na dua, Imam Hussein (A.S) huitwa kuwa yeye ni:
    1_"Mlango wa rehema pana ya Mwenyezi Mungu"
    2_"Mlango wa wokovu wa Umma".
  • Imam Hussein (as), alikuwa na huruma hata kwa maadui zake. Kwa Mfano:
    • Msimamo wake wa huruma kwa Hurru bin Yazid Al_Riyahi na
    • Ukarimu wake kwa Ubaydullah bin al-Hurr al-Ju'fi, licha ya kukataa kuungana naye.
  • Imam Hussein (A.S) alilia siku ya A'shura, na hakulia kwa ajili ya Nafsi yake, bali kwa ajili ya maadui wake ambapo aliwahurumia kuwa wataingia Motoni kwa kumuua.

    Madrasat Hazrat Zainab (SA) - Kigamboni | Imam Hussein (A.S) ni Mlango wa Rehema Pana ya Mwenyezi Mungu

🔹 Sehemu ya Tatu 

Kisa cha Mtoto Ali Asghar (A.S)

  • Imam Hussein (A.S) alikuwa na watoto watatu walioitwa Ali:
    • Ali Akbar,
    • Ali ibn al-Hussein (Imam Sajjad), na
    • Ali Asghar (mtoto mchanga).
  • Katika hali ya mwisho ya mapambano, alimleta Ali Asghar uwanjani akiwa na kiu kali ili kumuombea ya kunywa kwa Maadui waliokuwa wamezingira Mto Furati.
    Alisema: "Kama humnitaki mimi, basi mhurumieni mtoto huyu."
  • Lakini adui alimrushia mshale wa sumu wenye ncha mbili, ukamchoma shingoni kutoka sikio moja hadi jingine. Imam (as) alilia na mikono yake ikajaa Damu ya Mwanae, na akarusha damu hiyo na kumwambia Mwenyezi Mungu:
    "Ewe Mola! Hukumu baina yetu na watu hawa waliotuita lakini sasa wanatuua."

    Madrasat Hazrat Zainab (SA) - Kigamboni | Imam Hussein (A.S) ni Mlango wa Rehema Pana ya Mwenyezi Mungu

🔹 Sehemu ya nne

Wito kwa Waislamu

  • Kuwa na Taq'wa ni jambo bora zaidi la kumridhisha Allah.
  • Maimamu na watu wa Allah wote walifikia vyeo vya juu kwa kupitia Qur'an na toba na kufanya Tawassul kupitia Imam Hussein (A.S).
  • Ziarat ya A'shura kila siku ilikuwa njia ya kupata nuru ya kiroho.

Madrasat Hazrat Zainab (SA) - Kigamboni | Imam Hussein (A.S) ni Mlango wa Rehema Pana ya Mwenyezi Mungu

Hitimisho:

Imam Hussein (A.S) alikuwa ni mfano wa rehema ya Mwenyezi Mungu Duniani. Mapambano na msimamo wake ni darasa kwa Umma wote wa Mwanadamu.
Kwa Mantiki hiyo:
1_ Waislamu waitikie wito wa Imam Hussein (A.S).
2_ Waonyeshe huruma kwa wengine.
3_Watubu na wafanye toba, na Tawassul kwa kupitia kwa Ahlul-Bayt Rasulillah (amani iwe juu yao), ili kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu.


Wallahamdulillah Rabbil A'alamina

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha